Ezekiel 45:1-4

Mgawanyo Wa Nchi

1 a“ ‘Mtakapogawa nchi kuwa urithi, mtaitoa sehemu ya nchi kwa Bwana kuwa eneo takatifu, urefu wake dhiraa 25,000,
Dhiraa 25,000 ni sawa na kilomita 11.25.
upana wake dhiraa 20,000
Dhiraa 20,000 ni sawa na kilomita 9.
eneo hili lote litakuwa takatifu.
2 dKatika hiyo, itakuwepo sehemu mraba ambayo ni mahali patakatifu kila upande dhiraa 500 ikiwa imezungukwa na eneo la wazi lenye upana wa dhiraa hamsini. 3 eKatika eneo takatifu, pima sehemu yenye urefu wa dhiraa 25,000 na upana wa dhiraa 10,000.
Dhiraa 10,000 ni sawa na kilomita 4.5.
Ndani ya hilo eneo kutakuwa mahali patakatifu, Patakatifu pa Patakatifu.
4 gItakuwa sehemu takatifu ya nchi kwa ajili ya makuhani, wale wanaohudumu ndani ya mahali patakatifu na ambao hukaribia ili kuhudumu mbele za Bwana. Patakuwa mahali pa nyumba zao pamoja na sehemu kwa ajili ya mahali patakatifu.
Copyright information for SwhNEN